BUKOBA SPORTS

Saturday, July 26, 2014

JOSE MOURINHO AANZA MAJIGAMBO!! ADAI SHAW ANGEIVURUGA CHELSEA, LOUIS VAN GAAL AMPUUZA!! ANENA NA KUDAI IPO SIKU WATAKUTANA USO KWA USO!!

MENEJA wa Chelsea, José Mourinho, ameanza kumchimba mkwala Bosi wake wa zamani Louis van Gaal kwa kuipiga vijembe Man United na kudai Mchezaji mpya wa Manchester United Luke Shaw ni ‘Bei ghali’ na angeivuruga Chelsea.
Mourinho alikuwa anataka kumchukua Beki huyo mwenye Miaka 19 lakini Mchezaji huyo akaichagua Man United ambao walimnunua kwa Pauni Milioni 27 kutoka Southampton na kumpa Mshahara wa Pauni Laki Moja.
Baada ya kumkosa Shaw, Mourinho akamnunua Mbrazil Filipe Luís kutoka Atlético Madrid.

Lakini Mourinho amedai: “Kama tukimlipa Kijana wa Miaka 19 Fedha ya aina ile tutavunja utulivu wetu na kuleta mzozo. Wachezaji wengine wangekuja na kudai kwanini huyu analipwa hivyo wakati mimi nimecheza Mechi 200 na kuleta Mataji silipwi hivyo!”

Mourinho aliongeza: “Klabu nyingine ikilipa hivyo ni shauri yao. Sisi tumempata Luis kwa Bei poa!”Wanahabari walipomhoji Meneja wa Man United, Louis van Gaal, kuhusu kauli ya Mourinho, Mdachi huyo ambae alikuwa Bosi wa Mourinho walipokuwa wote Barcelona, alijibu hawezi kujibu kupitia vyombo vya habari bali atamjibu Mourinho uso kwa uso.

No comments:

Post a Comment