BUKOBA SPORTS

Monday, August 25, 2014

LA LIGA: BARCELONA 3 vs 0 ELCHE, LIONEL MESSI AANZA MSIMU MPYA NA BAO MBILI!!

BAO za Barcelona zilifungwa na Lionel Messi dakika ya 42 kipindi cha kwanza na bao la pili likifungwa na Munir El Haddadi katika dakika ya 46 na pia Lionel Messi aliongeza bao lake la pili katika dakika ya 63 kipindi cha pili na kufanya bao kuwa 3-0 dhidi ya Elche. Mechi hii hawakuimaliza wote 11 Barcelona kipindi cha kwanza dakika ya 44 Javier Mascherano alifanya rafu mbaya kwa mchezaji wa Elche kwa kumtega kwa nyuma wakati anakimbia na mpira kwenda kufunga bao na Mwamuzi kumwonesha kadi nyekundu.Lionel Messi akishangilia moja ya bao lake usiku huu dhidi ya Elche
 Munir akipongezwa na  Jordi Alba baada ya kuifungia bao  Barcelona
Pishaaaa!!
Messi na Jordi Alba wakishangilia Ushindi
Munir akipongezwa na wenzie baada ya kufunga bao
Munir akishangilia bao lao la pili barcelona kwenye uwanja wao  Nou Camp usiku huu kwenye mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Spain La Liga!

No comments:

Post a Comment