BUKOBA SPORTS

Sunday, August 24, 2014

ANGEL DI MARIA AAGA WACHEZAJI WA REAL MADRID LEO! UNITED YAKUBALIANA DAU LA £63.9M NA REAL!

Manchester United wamekamilisha mazungumzo na Real Madrid na kukubaliana kulipa Dau la Pauni Milioni 63.9 kumnunua Angel Di Maria ambayo ni Rekodi kwa Uingereza.
Jumatatu, Di Maria anatarajiwa kutua Jiji la Manchester kwa mazungumzo ya mwisho na kujitayarisha kuikabili Burnley kwenye Mechi ya Ligi huko Turf Moor Jumamosi ijayo.

Ada hii ya Uhamisho wa Di Maria itavunja Rekodi ya Ununuzi wa Bei ghali wa Fernando Torres ambayo Chelsea walilipa Pauni Milioni 50 kumnunua kutoka Liverpool Miaka Mitatu iliyopita.
di maria argentina
Kwa mujibu wa Kituo cha TV cha Sky Sports, kupitia Mdadisi wao na Mtaalam wa Masuala ya Soka ya Spain, Guillem Balague, Man United walitoa Ofa ya Euro Milioni 60 na Real kutaka Euro Milioni 90 na hatimae kukubaliana Euro Milioni 80 ambazo ni sawa na Pauni Milioni 63.9.
Left out: Di Maria, pictured during the first leg of the Spanish Super Cup, did not make the squad for the second leg against rivals Atletico Madrid
Mara baada ya Leo kutoka Sare 1-1 na Sunderland huko Stadium of Light, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, aliulizwa kuhusu Di Maria na akajibu: “Klabu inapaswa kutangaza. Ikiwa mambo tayari tutakuja na kuwaambia safi! Kwa sasa hatusemi lolote!”

Alipoulizwa moja kwa moja kama angependa kumsaini Di Maria, Van Gaal alijibu ndiyo na kuongeza: “Pia nampenda Messi na nampenda Vidal na wapo Wachezaji wengi Duniani nawapenda lakini wote hawawezi kuja Manchester United!”

Huko Madrid hii Leo, Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amethibitisha kuondoka kwa Angel Di Maria na kusema alikwenda Kituo cha Mazoezi kuaaga wenzake.

No comments:

Post a Comment