
Mata akishangilia bao lake

1-0 Mata anaipachikia bao United.
Dakika ya 17 kipindi cha kwanza Juan Mata anaifungia bao la kwanza Manchester United baada ya kazi nzuri ya Valencia kutoa krosi iliyowapita mabeki wa Sunderland na hatimae Mata kuupata mpira huo na kufunga bao.
Dakika ya 30 Jack Rodwell anaisawazishia bao kwa kichwa Sunderland baada ya kupigwa kona na Sebastian Larsson.
Wayne Rooney hoi baada ya Bao kurudi!!

Taswira kamili!! Viongozi wa United akiwemo Meneja wao Van Gaal

Kwa Mwamuzi wakiteta jambo..

Wayne Rooney hoi!!
Wakikabiliwa na Majeruhi wengi na pia kushindwa kumchezesha Mchezaji wao mpya Beki Marcos Rojo kutokana na kuchelewa kupata Kibali cha Kazi cha Nchini Uingereza, Man United hii Leo walianza vizuri kwa kufunga Bao katika Dakika ya 17 kupitia Juan Mata baada ya pasi ya Antonio Valencia.

Gus Poyet wa Sunderland akibwatuka!

Manchester United walifungwa mechi ya Ufunguzi na swansea City bao 2-1 Old trafford na sasa wanataka kurudi upya ugenini kati yao na Sunderland kwenye mechi ya raundi ya pili.

Kazi ipo...nani kuibuka kidedea..

Danny Welbeck na wenzake wakiingia kwenye Uwanja wa Sunderland tayari kwa kukipiga na Sunderland jioni hii.

Return: Robin van Persie anatarajia kucheza nae baada ya mapumziko marefu ya Kombe la Dunia, anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza katika msimu huu mpya 2014/15 tangu uanze wiki iliyopita.

Meneja wa Sunderland Gus Poyet

Louis van Gaal akimwaga wino kwa mashabiki

Robin van Persie kuanza katika kipute cha leo baada ya kutoka kwenye mapumziko.
No comments:
Post a Comment