BAO 2 ndani ya Dakika 3 za kwanza ziliwapa Chelsea mwanzo mzuri Ugenini huko Goodison na Chelsea wakamaliza Mechi hii kwa ushindi wa Bao 6-3.
Bao hizo za mapema za Chelsea, zenye utata wa Ofsaidi, zilifungwa na Diego Costa na Ivanovic.
Everton walipata Bao lao la kwanza katika Dakia ya 45 kupitia Mirallas.
Hadi Mapumziko Chelsea 2 Everton 1.
Kipindi cha Pili, Chelsea walipiga Bao la 3 mfungaji akiwa Coleman, alirjifunga mwenyewe, na Naismith kuipa Everton Dakika 2 baadae lakini Chelsea wakapiga Bao la Nne kupitia Matic na Dakika 2 baadae Mchezaji mpya wa Everton, Samuel Eto’o akaipigia Everton Bao la 3.
Huku Gemu ikiwa 4-3, Ramires akaipa Chelsea Bao la 5 katika Dakika ya 76 na Diego Costa akapiga Bao la 6 kuikata maini Everton.
Mapema Diego Costa aliifungia bao ndani ya dakika 1 ya kwanza na hapa akipongezwa na John Terry.
Bao la pili lilifungwa na Branislav Ivanovic katika dakika ya tatu 3'
No comments:
Post a Comment