BUKOBA SPORTS

Tuesday, August 26, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO JUMANNE NA KESHO JUMATANO MITANANGE KUPIGWA KUTAFUTA TIMU 10.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kwenye Mkutano na waandishi wa Habari juu ya Mchezo wa wa kesho na Besiktas ambao walitoka sare ya bila kufungana wiki liyopita.Giroud kuukosa mtananange huo wa kesho kwenye marudiano baada ya kuumia.
 DROO ya kupanga hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI,  itafanyika Ijumaa huko Monaco na tayari zipo Timu 22 ambazo zipo ndani yake, wakiwemo Mabingwa Real Madrid, lakini Timu nyingine 10 zilizobaki zitajulikana leo Jumanne na kesho Jumatano Usiku baada ya Mechi za Marudiano za Raundi ya Mwisho ya Mchujo.
Droo hiyo ya Makundi itajumuisha jumla ya Timu 32 ambazo zitapangwa Makundi 8 ya Timu 4 kila moja huku Timu za Nchi moja zikitengwa na kuwa Makundi tofauti.
Jumanne Usiku zipo Mechi 5 za Marudiano na ni Timu za Zenit St Petersburg ya Urusi na FC Porto ya Ureno ndizo zenye nafuu kidogo baada ya kushinda Mechi zao za Ugenini zote kwa Bao 1-0.
FC Porto watakuwa Nyumbani kurudiana na Lille ya France na vile vile Zenit St Petersburg wako kwao kucheza na Standard Liège .
Jumatano pia zipo Mechi 5 na Timu yenye nafuu pekee kwa kushinda Mechi yao ya kwanza ya Ugenini ni Bayer 04 Leverkusen ya Germany ambayo iliichapa FC Copenhagen Bao 3-2.
Ludogorets Razgrad ya Bulgaria na Malmö FF ya Sweden zipo Nyumbani lakini zina kazi ngumu ya kupindua vipigo vya Ugenini.
Kwenye Mechi nyingine za Marudiano, Athletic Bilbao ya Spain ipo Nyumbani kucheza na Napoli ya Italy baada ya kutoka 1-1 na Arsenal ya England itakuwa kwao Emirates kurudiana na Besiktas ya Urusi baada kutoka 0-0 huko Uturuki na pia kumaliza Mechi hiyo wakiwa Mtu 10 baada ya Aaron Ramsey kupewa Kadi Nyekundu na hivyo sasa kuikosa Mechi hii.
Timu 10 ambazo zitashindwa kwenda Makundi ya UCL zitatupwa kwenye Mashindano ya UEFA EUROPA LIGI hatua ya Makundi.


UEFA CHAMPIONS LIGI
RAUNDI YA MWISHO MCHUJO

Jumanne Agosti 26

19:00 Zenit St Petersburg v Standard Liège [1-0]
Apoel Nicosia v Aalborg BK [1-1]
BATE Borisov v Slovan Bratislava [1-1]
Celtic v NK Maribor [1-1]
FC Porto v Lille [1-0]


Jumatano Agosti 27
Arsenal v Besiktas [0-0]
Athletic Bilbao v Napoli [1-1]
Bayer 04 Leverkusen v FC Copenhagen [3-2]
Ludogorets Razgrad v Steaua Bucharest [0-1]
Malmö FF v FC Red Bull Salzburg [1-2]

No comments:

Post a Comment