Di Maria akiingia kwenye imaya ya Man United kwenye sehemu yao ya Mazoezi Carrington.
Angel Di Maria alipotembelea uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington jana jioni kabla ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Real Madrid kwa pauni milioni 59.7
Di Maria kwenye siti ya nyuma akiingia
Di Maria Anaungana na Marcos Rojo, Ander Herrera pamoja na Luke Shaw ambao ndio tayari wamesainiwa na Man United Msimu huu wa 2014/15
Winga huyo wa Argentina, mwenye Miaka 26, Leo Asubuhi atafanyiwa upimwaji afya yake na kusaini Mkataba akiwa tayari kucheza Mechi yake ya kwanza hapo Jumamosi wakati Man United watakapokuwa Ugenini kucheza na Burnley kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Uhamisho huu wa Di Maria umeifanya Man United itumie Jumla ya Pauni Milioni 132 kusaini Wachezaji wapya katika kipindi hiki cha Uhamisho.
Wachezaji wengine walionunuliwa na Man United katika kipindi hiki ni Fulbeki wa Kushoto Luke Shaw, Kiungo Ander Herrera na Mchezaji mwingine wa Argentina Marcos Rojo walionunuliwa kwa Jumla ya Pauni Milioni 72.
Uhamisho wa Di Maria umevunja ile Rekodi iliyowekwa na Chelsea Mwaka 2011 walipomnunua Fernando Torres kutoka Liverpool kwa Pauni Milioni 50.
No comments:
Post a Comment