Mario Balotelli akipongezwa baada ya kusawazisha bao dakika ya 86.Liverpool walipigana mpaka dakika za mwisho na kuweza kuifunga Swansea katika dakika za lala salama.Marvin Emnes aliwachapa bao kipindi cha pili dakika ya 65 na kufanya waongoze bao hilo mpaka dakika ya 86 Mario Balotelli alipowanusuru Liverpool kwenye Uwanja wao Anfield kwa kuwasawazishia na kufanya 1-1. Zikiwa zimebaki dakika za nyongeza mpira kumalizika Dejan Lovren aliwafungia Liverpool bao la kichwa kwa mpira wa kupigwa frii kiki na kumaliza mpira Liverpool wakiwa juu ya bao 2-1. Swansea City walibaki 10 Uwanjani baada ya mchezaji wao kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumkwatua mchezaji wa Liverpool chini.Mario alipowaokoa Liverpool kwa kusawazisha bao dakika ya 86 na kufanya 1-1.
No comments:
Post a Comment