Didier Drogba akishangilia bao lake la kwanza kwa Chelsea.Kipindi cha pili dakika ya 48 Drogba aliwapachikia bao la kwanza Chelsea na kufanya 1-0 dhidi ya Wenyeji Shrewsbury. Dakika ya 77 Andrew Mangan aliisawazishia bao Shrewsbury Town kwa kufanya 1-1. Chelsea waliongea bidii na kubadilisha wachezaji kwa kumweka Willium alisababisha bao la pili kufungwa wakijifunga wenyewe Shrewsbury Town kupitia kwa kichwa cha Jermaine Grandison dakika ya 81 na kufanya 2-1. Na mtanange kumalizika Chelsea wakiwa kidedea kwa ushindi wa bao 2-1.
No comments:
Post a Comment