BUKOBA SPORTS

Wednesday, October 29, 2014

YANGA YAWEKA KAMBI KAHAMA,KUKIPIGA NA AMBASSADOR LEO, MAXIMO AAPA LAZIMA WAIUE KAGERA SUGAR JUMAMOSI

Kikosi cha Young Africans kimewasili jana mjini Kahama ambapo kitaweka kambi ya siku ya tatu kabla ya kuelekea mjini Bukoba kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara siku ya jumamosi dhidi ya wenyeji timu ya Kagera Sugar.
Young Africans ikiwa mjini Kahama itacheza mchezo wa kirafiki siku ya jumatano dhidi ya wenyeji timu ya Ambassador FC ikiwa ni sehem ya maandalizi ya kocha kuelekea mchezo wa wakata miwa wa mkoa Kagera.
Kocha Marcio Maximo leo asubuhi amekiongoza kikosi chake kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa mjini hapa ikiwa ni maandalizi ya mechi ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Kagera Sugar baada ya kupata pointi tatu katika mchezo dhidi ya Stand United.
Katika mazoezi yalioyofanyika leo asubuhi, wachezaji 28 waliombatana na kikosi cha Young Africans wamefanya mazoezi, huku kocha mkuu Maximo akisema vijana wake baada ya kupumzika kwa siku ya jana (jumapili) sasa wataendelea na mazoezi kila siku asubuhi na jioni kwa siku mbili.

"Mechi yetu dhidi ya timu ya Stand United ilikuwa nzuri, tukapata pointi tatu ambazo zimetuongezea morali ya ushindi ugenini, na kwa sasa tunajipanga pia kupata ushindi dhidi ya timu ya Kagera Sugar,"alisema Maximo.

Aliongeza: "Kwa sasa nguvu zetu zote tunazielekezea kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar siku ya jumamosi, na vijana wako fit, ari na morali ya kusaka pointi tatu."

No comments:

Post a Comment