KANUNI ya Meneja mpya wa Manchester United, Luis van Gaal, kuwatumia Chipukizi wa Old Trafford imeifanya Timu hiyo ikamate Nafasi ya Pili Barani Ulaya kwa kutumia Wachezaji Chipukizi ambao vipaji vyao vimekuzwa humo humo ndani ya Klabu.
Timu iliyo juu ya Man United ni Barcelona ambayo Van Gaal aliwahi kuifundisha na ni yeye ndie aliewapa nafasi Nyota wao wa sasa, Xavi na Andres Iniesta, kuichezea Timu ya Kwanza ya Barcelona kwa mara ya kwanza kabisa.
Wakati Barcelona ina jumla ya Wachezaji 43 ambao walikuzwa vipaji vyao Klabuni humo, Man United inao 36 wakifuatiwa na Real Madrid wenye 34, Lyon 33, PSG 27 na mkiani, kwenye Listi ya Klabu 51 Barani Ulaya, wapo Mabingwa wa England Man City wenye na Mchezaji mmoja tu wa Nyumbani kwenye Kikosi chao cha sasa na 11 wakiwa Klabu nyingine.
Takwimu hizi zimeratibiwa na CIES, International Centre for Sports Studies, ambacho ni Kituo Maalum cha Mafunzo kilichopo huko Neuchâtel, Switzerland kilichoanzishwa Mwaka 1995 kwa ushirikiano wa FIFA, Chuo Kikuu cha Neuchâtel na Mamlaka za Mji na Jimbo la Neuchâtel.
Kwa mujibu wa Takwimu hizo za CIES, Wachezaji waliokuzwa vipaji Nyumbani ni wale ambao bado wapo kwenye Klabu zao na wengine ambao wameuzwa au wako kwa Mkopo kwenye Klabu nyingine lakini wanachezea Ligi kubwa Ulaya ambazo ni Ligi Kuu England, La Liga ya Spain, Bundesliga ya Germany, Serie A ya Italy na Ligi 1 ya France.
Wiki iliyopita ilitobolewa kuwa Louis van Gaal alichezesha Kikosi chenye Chipukizi wengi na kukamata Nafasi ya Pili Barani Ulaya kwa kuwa na Wachezaji wa Umri mdogo walipocheza na kutoka Sare na WBA.
Tangu atue Old Trafford Msimu huu, Van Gaal ameshatoa nafasi kwa Chipukizi 7 kuichezea kwa mara ya kwanza Timu ya Kwanza ya Man United.
Chipukizi hao ni Tyler Blackett na Jesse Lingard waliocheza Mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Swansea City, Saidy Janko, Reece James na Andreas Pereira waliocheza Mechi ya Capital One Cup dhidi ya MK Dons na Paddy NcNair aliecheza Mechi na West Ham na baadae kwenye Mechi hiyo hiyo kuingia Tom Thorpe.

Top 10
At the club | At another 'big 5' club | Total | ||
1 | Barcelona | 13 | 30 | 43 |
2 | Manchester United | 12 | 24 | 36 |
3 | Real Madrid | 8 | 26 | 34 |
4 | Lyon | 15 | 18 | 33 |
5 | Paris Saint Germain | 5 | 22 | 27 |
6 | Athletic Bilbao | 15 | 9 | 24 |
- | Real Sociedad | 15 | 9 | 24 |
- | Stade Rennais | 5 | 19 | 24 |
9 | Bordeaux | 11 | 11 | 22 |
- | Lens | 9 | 13 | 22 |
- | Arsenal | 7 | 15 | 22 |
- | Atalanta | 5 | 17 | 22 |
No comments:
Post a Comment