BUKOBA SPORTS

Tuesday, October 28, 2014

RONALDO NDIE MCHEZAJI BORA LA LIGA, AMFUNIKA LIONEL MESSI!!

Cristiano Ronaldo is primed to clinch a second consecutive Ballon d'Or after beating Lionel Messi to the top prize in Spain
CRISTIANO RONALDO amezoa Tuzo ya Mchezaji Bora ya Chama cha Soka Spain, LFP, [Liga de Fútbol Profesional] kwa kung’ara kwenye La Liga kwa Msimu wa 2013/14.
Kwenye Msimu huo, Ronaldo alipachika Bao 31 kwenye Mechi 30 za La Liga.
Ronaldo, ambae pia ndie Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, Ballon d'Or, anakuwa Mchezaji wa Pili kutwaa Tuzo hii ya LFP ambayo ilianzishwa Msimu wa 2008/09 na tangu wakati huo Tuzo zake zote kubebwa na Mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi.
Safari hii, Lionel Messi hakuambua Tuzo yeyote kwa Msimu wa 2013/14 wa La Liga ambao Sherehe zake zilifanyika Jana.
Ronaldo, ambae pia alitajwa kuwa ndie Fowadi Bora wa la Liga kwa Msimu wa 2013/14, alitoa shukran kwa kusema: “Ninapaswa kuwashukuru Wachezaji wenzangu, Real Madrid, Familia yangu…huu ni wakati mzuri katika maisha yangu ya Soka.”
Mbali ya kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora na Fowadi Bora, Ronaldo pia alitwaa ile ya Goli Bora kwa Bao lake dhidi ya Valencia katika Wiki ya 36 ya La Liga.

Diego Simeone wa Mabingwa Atletico Madrid ndie alietwaa Tuzo ya Kocha Bora wakati Tuzo ya Mchezaji Bora toka Afrika aliitwaa Mchezaji kutoka Algeria Yacine Brahimi wa Klabu ya Granada.

No comments:

Post a Comment