BUKOBA SPORTS

Saturday, October 25, 2014

EL CLASICO: REAL MADRID 3 v 1 BARCELONA, CRISTIANO RONALDO, PEPE NA KARIM BENZEMA WAWANYOOSHA BARCA!! BADO POINTI MOJA TU KILELENI!

Lionel Messi hoi leo kwenye El Clasico. (kulia) ni Wachezaji wa Real wakipongezana baada ya kuwashona bao 3-1 Barcelona na kupanda hadi nafasi ya pili wakiwa natofauti ya pointi 1 tu na Vinara Barca waliopo kileleni wakiwa na pointi 22.Cristiano Ronaldo akipongezana na james kwenye Uwanja wa Estadio Santiago BernabéuCristiano Ronaldo kwenye patashika!
Kipindi cha pili dakika ya 50 Pepe ndie aliyetupia kambani bao la pili na kufanya Real kuongoza 2-1 dhidi ya Barcelona akipewa pasi na Toni Kroos. 
Dakika ya 61 Karim Benzema aliifungia bao la tatu Real na kufanya 3-1 dhidi ya Barcelona. Ni baada ya kuwatoka Mabeki wa Barcelona na kutokea chenga safi ya James Rodríguez na kumwachia Karim Benzema aliyemaliza kazi kwa kuziona nyavu na kupata bao la tatu kwenye Uwanja wa Estadio Santiago Bernabéu wakiongozwa na mwamuzi Jesús Gil na mbele ya mashabiki wapatao 85450.
Ushindi huu unawapandisha Real nafasi ya pili wakiwa na pointi 21 nyuma ya pointi moja ya Vinara Barca ambao wana pointi 22 kileleni.Neymar ndiye aliyeifungia bao Barcelona dakika ya 4 kipindi cha kwanza na kuifanya Barca kuongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Real Madrid.
1-1 Cristiano Ronaldo anaswazisha kwa mkwaju wa Penati katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza. Ni baada ya Piqué Kuunawa mpira uliopigwa na Marcelo ndani ya kumi na 18 (Box). Hadi Mapumziko Real madrid 1, Barcelona 1.
Mechi ya kwanza kuichezea Barcelona leo, Suarez akiwapongeza na kusalimiana na Mashabiki wake

VIKOSI:
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo, Kroos, Modric, Isco, James, Ronaldo, Benzema
Akiba: Navas, Varane, Khedira, Hernandez, Arbeloa, Nacho, Illarramendi
Barcelona: Bravo; Alves, Piqué, Mascherano, Mathieu; Xavi, Busquets, Iniesta; Messi, Suarez, Neymar
Akiba: Ter Stegen, Rakitic, Pedro, Bartra, Alba, Roberto, Munir
Taswira ya Mashabi kuelekea mtanange wa El Clasico

No comments:

Post a Comment