BUKOBA SPORTS

Thursday, October 2, 2014

EUROPA LEAGUE: KRASNODAR 1 vs 1 EVERTON, SAMUEL ETO'O AIOKOA KIPIGO EVERTON!


Samuel Eto'o  akishangilia bao lake la dakika za mwisho kwenye dakika ya 82 baada ya kuisawazishia bao  Everton kwa kuweka 1-1 dhidi ya  Krasnodar na mpira huo kumaliza kwa sare hiyo.

Eto'o aliweka sare hiyo huku kipute hicho kikionekana kuelemea upande mmoja na kuonekana kama mpira huo ungelimalizika kwa 1-0 lakini la!

Patashika kwenye lango Wachezaji wa  Everton wakionekana kufanya bidii ya kutafuta bao

Mchezaji wa Krasnodar Ari ndie aliyewafungia bao hilo na kufanya  1-0  kipindi cha kwanza dakika ya  42 kwenye Uwanja wa  Kuban.

Ariakishangilia na kupongezwa na kocha Oleg Kononov kwenye Europa ligi Kundi H ambapo wao
Everton walishinda Mechi yao ya kwanza bao 4-1 dhidi ya Klabu ya Germany Wolfsburg, Na leo hii walikuwa Ugenini kucheza na FK Krasnodar ya Urusi ambako wamemaliza mtanange huu kwa sare ya 1-1 na mchezo wa kwanza wa timu hiyo ya Urusi walitoka sare pia ya bao 1-1.

aliyewapa bao Krasnodar Ari akishangilia bo lake la dakika ya 42.

Kipa wa Everton  Tim Howard akishangilia bao baada ya kusawazisha timu yao kwa kuweka 1-1

Patashika likiendelea...

Mashabiki wa Urusi wakiipamba FC Krasnodar

Phil Jagielka akichuana na mchezaji wa  Krasnodor Ricardo Laborde  kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment