BUKOBA SPORTS

Friday, November 7, 2014

DIAFRA SAKHO AWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI OCTOBA LIGI KUU ENGLAND, ALLARDYCE NAE KOCHA BORA WOTE KUTOKA WEST HAM

WASHINDI wa tuzo za Ligi Kuu ya England Oktoba, wametajwa na mshambuliaji wa West Ham United, Diafra Sakho ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi huo.
Kocha wa West Ham United, Sam Allardyce pia ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi, akiwashinda kocha wa Hull City, Steve Bruce, Jose Mourinho wa Chelsea na Alan Pardew wa Newcastle United.
Sakho amekuwa katika kiwango kizuri The Hammers tangu ajiunge nayo kutoka Metz msimu huu na mwezi uliopita alifunga mabao matatu na kutoa pasi ya bao moja, West Ham ikizifunga QPR, Burnley na Manchester City.
Wengine walioingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hiyo ni Sergio Aguero wa Man City, Leighton Baines wa Everton, Saido Berahino wa West Bromwich Albion, Alexis Sanchez wa Arsenal na Dusan Tadic wa Southampton.
Diafra Sakho amekuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England Oktoba na kocha wake, Sam Allardyce nae amepewa nafasi hiyo kwa mwezi Octoba.

No comments:

Post a Comment