BUKOBA SPORTS

Friday, November 7, 2014

SASA NI HATARI TUPU ITALIA!! MWANAMITINDO CLAUDIA ROMANI KUPULIZA KIPENGA SERIE A NA SERIE B !


MWANAMITINDO wa Italia, Claudia Romani ameingia kwenye rani mpya katika ulimwengu wa soka- baada ya kufaulu mtihani wa kuwa refa wa kulipwa.
Kimwana huyo mwenye umri wa miaka 32 amevua viatu vyake vya mchuchumio ili awe refa, kitu ambacho imekuwa agenda yake kwa miezi kadhaa.

Romani sasa amefuzu kuwa refa wa mechi za Ligi Kuu ya Italia maarufu kama Serie A na Daraja la kwanza, maarufu kama Serie B - kitu ambacho anaelewa vizuri.


Claudio Romani sasa amekuwa refa ambaye amefuzu kuchezesha za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza Italia

Amesema: "Kukimbia uwanjani na wachezaji wote hao na kuchezesha mechi ni nafasi adimu,".
Hakuna mwanamke amewahi kuchezesha mechi ya Serie A hadi sasa kutokana na uzoefu, jambo ambalo linatarajiwa kubadilika karibuni kwa Romani kutazamiwa kuwasha moto katika ligi ya Italia.

No comments:

Post a Comment