Wachezaji Timu zote mbili Kagera Sugar na Yanga wakisalimiana kabla ya mtanange kuanza.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Klabu ya Dar es salaam Young Afrika imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji wao Kagera Sugar kwenye mchezo uliopigwa ndani ya Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.
Kipindi cha kwanza Timu zote mbili zilimaliza bila ya kufungana, Kipindi cha pili Kagera Sugar walitumia faida ya kucheza nyumbani na kufanikiwa kupata bao lililofungwa kiufundi na paul Ngwai na kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0 na kuwaacha Yanga wakibaki na pointi zao 10 ambazo wamevuna katika michezo 6.
Katika mchezo huo Mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Cannavaro baada ya kumpiga Kiwiko mchezaji wa Kagera Sugar.Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya timu ya Yanga kutoka Jijini dar es Salaam. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.comKikosi cha Yanga kilichoanza.Picha ya pamoja Timu kepteni na Waamuzi wa Mtanange KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Martinus Ignatus 'Mart Nooij nae alikuwepo uwanjani kaitaba kujionea kipute hicho.Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho kwenye Patashika na mchezaji wa Kagera SugarMshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho akimtoka mchezaji wa kagera Sugar.Mashabiki waliingia kwa Wingi leo kwenye Uwanja wa Kaitaba kujionea mtanange wa Kagera Sugar vs YangaTaswira ya Mashabiki kwenye Uwanja wa Kaitaba kwenye jukwaa dogoAndrey Coutinho akiwekwa chini ya Ulinzi na wachezaji wawili wa Kagera huku akionekana kuwazidi ujanja wenzake wa kagera.Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.comJaja akigombea mpira wa kichwaMashabiki wa timu ya Yanga wakiishangilia Timu yao waipendayoNdugu Chama Jumanne Chama Umande ambaye ni Katibu wa KRFA(kulia) akiwa amekaa na Kocha wa Timu ya Kagera Sugar Jackson Mayanja (kulia) wakiutazama mtanange.Kipindi cha pili Mtanange ulipamba moto. Ikawa ni kushmbuliana kwa zamu.Shabiki wa Yanga akiwa nje ya uzio wa Uwanja akifanya Yake Mchezaji wa kagera aliumia na hapa alikuwa akipewa msaada wa haraka na kipa wakeKipindi cha kwanza kilimalizika 0-0, lakini kipindi cha Pili Kagera walifanya shambulizi kali na kuifunga Yanga bao 1-0 bao lililofungwa na Paul Ngwai na kuweza kutangulia kwa bao hilo 1-0 mpaka mwisho wa dakika 90.Nadir Haroub "Cannavaro" akisindikizwa nje ya Uwanja baada ya kuondolewa kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Kadi hiyo ya Nadir Haroub ‘Cannavaro, imesababisha sintofahamu kwenye Kipute hicho Kaitaba, Haroub alipewa kadi nyekundu kwa kile alichojionea Mwenye Mwamuzi wa Mtanange wa leo kwa kumfanyia ndivyo sivyo Paul Ngwai aliyepachika bao la pekee katika Mtanange huo ambao Yanga Kalala kwa Bao 1-0 hapa Mjini Bukoba.
Mashabiki walibaki na maulizo na wengine wakipandwa na jaziba kutaka kuingia Uwanjani. Na baada ya Matange huo kumalizika Vurugu zilitokea za hapa na pale kwenye Uwanja wa kaitaba jambo ambalo limesababisha Askari kuwapa ulizi wa Kutosha Waamuzi hao. Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva akiondolewa kwenye Benchi la Ufundi na Mwamuzi wa mtanange huo baada ya kufanya kile ambacho si sawa kwa kuingia Uwanjani bila ruhusa ya Mwamuzi.Nje!! Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva akiondoka kwenye Benchi hilo la Ufundi machungu!Tegete aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho na hapa alikuwa akichuana na Benjami Asukile wa Kagera Sugar.Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange ndiye alikuwa kazini leo baada ya Kocha wao Jackson Mayanja kuwa nje kwenye Adhabu aliyopewa kwenye mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.comMshamabuliaji Geilson Santos Santana “Jaja” raia wa Brazil leo alibanwa sana. Akashindwa kutema cheche zake!Mchezaji wa Kagera chini!!!Dakika 90 zimemalizika!! 1-0Jaja, Niyonzimana Ngassa hoi!! Ni kipigo kwa timu Yanga. Yanga wamepoteza mchezo huu kwa kufungwa na Kagera Sugar bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba.KOCHA Mkuu wa Yanga Marcio Maximo akimnyooshea kidole Mwamuzi wa kati baada ya mpira kumalizika Kaitaba Jioni hii Baada ya kuchapwa bao 1-0.Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva na Marcio Maximo wote kwenye wakimtupia maneno Mwamuzi.Waamuzi wakiwa chini ya Ulinzi mali wa Polisi baada ya mchezo kumalizika.Mashabiki wa Yanga wakizozana na Mashabiki wa Kagera kwenye Uwanja wa Kaitaba. Jambo ambalo liliwabidi Askari kuingilia kati!!

No comments:
Post a Comment