Villa walibaki Mtu 10 baada ya Agbonlahor kupewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 65 na Refa Lee Mason kwa kumchezea Rafu Ashley Young.
Mara baada ya Mechi hiyo, Meneja wa Villa, Paul Lambert, alikaririwa akisema kuwa Agbonlahor hakustahili kutolewa na pia kudai Ashley Young alimwambia Kipa wa Villa Brad Guzan kwamba yeye ndie alimchezea Rafu Agbonlahor.
Hapo Jana, Villa walikata Rufaa kuipinga Kadi hiyo na hii Leo FA, Chama cha Soka cha England, kimeifuta lakini wameifungulia mashitaka Aston Villa kwa kosa la kudhibiti Wachezaji wao baada ya kumzunguka Refa Lee Mason alipotoa Kadi Nyekundi kwa Agbonlahor.
Villa imepewa hadi Jumatatu Desemba 30 Saa 3 Usiku kujibu Mashitaka yao.
Uamuzi huu wa FA wa kumfutia Kadi Agbonlahor unamaanisha atacheza Mechi ya Ugenini hapo Desemba 26 na Swansea City.
No comments:
Post a Comment