SIR ALEX AMSIFIA KOCHA VAN GAAL, ASEMA MAN UNITED ITARUDI KUWA TISHIO KAMA KAWAIDA YAKE CHINI YA KOCHA VAN GAAL, AMSIFIA PIA CARRICK KUWA NDIE KIUNGO KATI BORA UINGEREZA!
SIR Alex Ferguson amemsapoti Louis van Gaal na kudai atafanikiwa katika himaya yake Klabuni Manchester United huku akiamini chini ya Meneja huyo Wayne Rooney sasa yupo juu wakati Michael Carrick akidhihirisha ndie Kiungo wa Kati Bora Uingereza.
Akiongea kwenye Kipindi maalum kitakachorushwa Siku ya Krismasi na BT Sport, Ferguson alizungumzia pia himaya yake Man United.
Hivi sasa Man United wapo Nafasi ya Tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England tofauti na Msimu uliopita ambapo mrithi wa Ferguson, David Moyes, alishindwa kuiongoza vyema Timu.
Ferguson amesema: “Rooney amerejea, yupo juu na Rooney Siku zote atakufungia Magoli. Hilo ni jambo zuri ikiwa Timu ina mfungaji mahiri.”
Aliongeza: “Louis van Gaal- sijui anategemea vipi kupata matokeo mazuri wakati ana majeruhi kibao. Na akipata Wachezaji wote kwenye Timu, ichunge Man United. Kwa sababu yeye ni Kocha Bora, atafanya vyema!”
Sir Alex pia alifafanua kuhusu Wachezaji wapya walionunuliwa Msimu huu kwa kusema: “Siangalii nini kimetokea kwa Wachezaji wapya hivi sasa kwa sababu wanahitaji muda. Nilipowanunua Patrice Evra na Nemanja Vidic Mwezi Januari iliwachukua Miezi 5 kuzoea uchezaji wa Man United, kuzoea utamaduni, historia ya Klabu na Wachezaji hawa wapya itakuwa ni hivyo hivyo.”
Aliongeza: “United inao Wachezaji wazuri. Nadhani Michael Carrick ndie Kiungo Bora wa Kati kwa Uingereza, ni Mwingereza Bora katika Gemu. Robin van Persie, pengine Kombe la Dunia limemchosha lakini mwangalie kipindi cha pili cha Msimu, atakuwa safi. Lakini anaenikosha katika wote ni David de Gea. Tulipomleta hapa alikuwa Kinda lakini alikuwa na kipaji na nimefurahishwa nae sana!”
Pia Sir Alex Ferguson alidokeza kuwa Kikosi chake kilichotwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza kabisa akiwa na Man United ndicho chenye maana kubwa kwake na kueleza: “Watu wengi wanafafanua tofauti ya jinsi nilivyoitengeneza Man United katika Miaka 26 nikiwa na Wachezaji Bora kina Rooney, Ronaldo, Cantona, Keane, Robson, Schmeichel, yapo maongezi mengi sana. Lakini ukweli nadhani ari ya Man United imetokana na Timu ya Mwaka 1992. Hiyo iliwapa moyo kila Mtu Klabuni, si Mashabiki tu, mimi, Wafanyakazi wangu, Wakurugenzi, Bobby Charlton ambe alikuzwa na Matt Busby- ilirudisha historia ya Manchester United, bila ya wasiwasi!”
No comments:
Post a Comment