BUKOBA SPORTS

Monday, December 22, 2014

LIGI KUU ENGLAND: USIKU HUU NI PATASHIKA! STOKE CITY vs CHELSEA

Chelsea Usiku huu wanatua Britannia Stadium kucheza na Stoke City ambayo Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii waliibamiza Chelsea 3-2.
Baada ya kufungwa 2-1 na Newcastle, ikiwa Mechi yao ya kwanza kupoteza kwenye Ligi Msimu huu, Chelsea walirudi kwenye Reli kwa kuichapa Hull City 2-0 Wikiendi iliyopita.
Mechi hii ni muhimu mno kwa Chelsea hasa baada ya Mabingwa Watetezi Manchester City Jumamosi kuifunga Crystal Palace Ba0 3-0 na kuikamata Chelsea kwa Pointi kileleni wote wakiwa na Pointi 39.
Lakini Mechi hii na Stoke City ni Mechi moja mkononi kwa Chelsea ambao wakishinda watakuwa Pointi 3 mbele ya City huku Timu zote zikiwa zimecheza Mechi 17.
Tayari akionyesha wasiwasi kuhusu Mechi hii, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amemtaka Refa wa Mechi, Neil Swarbrick, kuwa makini na uchokozi wa Stoke City wanaosifika kwa kucheza nguvu kazi iliyojaa mabavu wakihamsishwa na kushabikiwa na Mashabiki wao zaidi ya 20,000 ndani ya Britannia ambao huwa wehu kwa kuishangilia Timu yao kichizi.
Mourinho aligusia kuhusu mpambano mkali unaotarajiwa Uwanjani kati ya Sentafowadi wake, Diego Costa, atakaekumbana na Sentahafu wa Stoke Ryan Shawcross ambae hana mzaha Uwanjani na hutumia kila mbinu kuwamudu Mastraika.
Mourinho amemtaka Refa Neil Swarbrick kuwa makini na kuchezesha kihaki bila kuhadaiwa na Wachezaji.
Jonathan Walters na Peter Crouch

No comments:

Post a Comment