BUKOBA SPORTS

Monday, December 22, 2014

RAIS KIKWETE AZUNGUMZA NA WAZEE LEO JIJINI. AKUBALI ANNA TIBAIJUKA KUPISHA!


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia.

Rais Jakaya Kiwete akihutubia taifa hii leo katika ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam kupitia wazee wa jiji hilo.

Pampoja na mambo mbalimbali Rais Kikwete amezungumzia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika nchini kote na kuunga mkono maamuzi ya Waziri TAMISEMI, Hawa Ghasia juu ya maamuzi ya kuwatimua kazi, kusimamisha, kuwashusha vyema na kuwapa maonyo ya madaraja mbalimbali watendaji wote waliohusika na kuharibika kwa uchaguzi huo katika maeneo yao.

Rais Kikwete hivi sasa anazungumzia sakata la ESCROW ambapo kwa mambo kadhaa ambayo yalikuwa yakisubiri uamuzi wake ikiwa ni pamoja na kuwaondoa mawaziri tajwa.

Rais Kikwete amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali tayari amejiuzulu, Bodi ya Tanesco imeshamaliza muda wake na tayari amesha teua Mwenyekiti Mpya wa Bodi huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akisema amesha zungumza nae na amemuomba apishe nafasi yake ateuliwe mtu mwingine.

Upande wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameomba amuweke kiporo yeye na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi dhidi yao.
Baadhi ya wazee na wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.

Wanahabari wakichukua kumbukumbu kwenye mkutano huo wa Mh.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo Desemba 22, 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitika wito wa kumsikiliza wakati wa kulihutubia Taifa kupitia Wazee kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ( Picha na Adam Mzee)
Baadhi ya Wanasiasa wakongwe waliohudhuria.
Kila wilaya ya mkoa wa Dar es salaam iliandaliwa sehemu maalum ya kukaa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alizungumzia uchaguzi na kutaka polisi kufanya kazi yao katika kuhakikisha uchaguzi ujao uchaguzi hauvurugwi na pia alifafanua mambo mbali mbali yaliyokuwa yakizungumziwa kuhusu akaunti ya ESCROW na kumwajibisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Ukumbi wa Diamond Jubilee ukiwa umefurika Wazee waliokuja kumsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
 kumbi ulifurika kila kona.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa ufafanuzi wa masula kadhaa yaliyoleta mkanganyiko kwenye sakata la Escrow Akaunti.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akipanga makaratasi yenye hotuba yake wakati wa kuhutubia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.

Wananchi wakishangilia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhitimisha hotuba yake kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza na Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alimpa taarifa Mheshimiwa Rais juu ya mafanikio ya ujenzi wa maabara katika Shule za Sekondari mjini Dar es Salaam pamoja na matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaaBofya Link hiyo kumsikiliza
http://www.ikulu.go.tz/

No comments:

Post a Comment