BUKOBA SPORTS

Wednesday, January 28, 2015

FULL TIME: SIMBA SC 1 vs 2 MBEYA CITY


Ligi kuu VODACOM imendelea Leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa Mechi pekee ambayo Simba ilichapwa 2-1 Mbeya City lakini stori kubwa ni Simba kukosa Penati Dakika ya mwisho ambayo ingewapa Sare.
Simba walitangulia kufunga Bao katika Dakika za Majeruhi za Kipindi cha Kwanza kwa Frikiki ya Ibrahim Hajib na Mbeya City kusawazisha Dakika ya 77 Mfungaji akiwa Hamad Kibopile.
Mbeya walipata Bao lao la ushindi Dakika za Majeruhi kwa Penati iliyofungwa na Yusuf Abdallah kufuatia Kipa Peter Manyika kumchezea Rafu Raphael Daudi.
Mara tu baada ya Bao hilo Simba walipata nafasi ya kutoka Sare baada ya Refa Abadallah Kambua kutoa Penati kwa Rafu aliyochezewa Jonas Mkude lakini Nassor Masoud ‘Chollo’ alifumua Shuti lililopiga Posti na kuleta kizaazaa kwa Mashabiki wa Simba.
Matokeo haya yameiacha Simba ikiwa Nafasi ya 11, 4 tu toka mkiani na Mbeya City kukwea hadi Nafasi ya 7.
Mechi zinazofuata za VPL zitachezwa Jumamosi na Jumapili.


Mlizinzi wa kati wa Simba SC, Hassani Isiacka akijaribu kujirinda kwa kumvuta jezi mmoja wa washambuliaji wa timu ya Mbeya City, jana ndani ya Uwanja wa Taifa jiji Dar, ambapo Simba ililala kwa mabao 2-1.

Mambo yalikuwa hivi

Baadhi ya mashabiki wa timu ya Mbeya City

Wachezaji wa Mbeya City wakiwa wamembeba kocha wao.

Shangwe za Mbeya City zikiendelea nje ya Uwanja muda mfupi baada ya kumalizika kwa mpambano huo.
Mlizinzi wa kati wa Simba SC, Hassani Isiacka akijaribu kujirinda kwa kumvuta jezi mmoja wa washambuliaji wa timu ya Mbeya City, jana ndani ya Uwanja wa Taifa jiji Dar, ambapo Simba ililala kwa mabao 2-1. Mambo yalikuwa hivi Baadhi ya mashabiki wa timu ya Mbeya City Wachezaji wa Mbeya City wakiwa wamembeba kocha wao. Shangwe za Mbeya City zikiendelea nje ya Uwanja muda mfupi baada ya kumalizika kwa mpambano huo. You might also like: AIRTEL NA UNESCO KUZINDUA RADIO ZA JAMII ARUSHA VIJIJINI - ... MAAJABU: MTOTO AZALIWA NA MAKALIO MATATU, MAMA YAKE ALIA ... JACK PATRICK NUSU AMTOE ROHO MTU SOFAPAKA YATAKA KOCHA MTANZANIA AU MWINGINE YEYOTE KUTOKA ... Dk Slaa amlipua Rais Jakaya Kikwete Linkwithin Posted by Musa Shigela at 10:58 PM Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Newer Post Older Post Home Subscribe to: Post Comments (Atom) POSTED TITLE Related Posts Plugin for WordPress, Blogger... TANZANIA ONE - MUSA MATEJA View my complete profile Search

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

No comments:

Post a Comment