Ghana walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa South Africa Bao 2-1 katika Mechi ya Kundi C la AFCON 2015.
South Africa walipata Bao katika Dakika ya 17 baada ya Mandla Masango kufuatia uzembe wa Ghana kuosha Mpira uliotumbukizwa ndani ya Boksi.
Hadi Mapumziko South Africa 1 Ghana 0.
Kipindi cha Pili Ghana walicharuka na hatimae kupata Bao Dakika ya 73 Mfungaji akiwa John Boye na kuongeza la pili kupitia Andre Ayew kwa Kichwa Dakika ya 83 alipounganisha Mpira wa Baba.
Ghana wamesonga Robo Fainali wakiwa Washindi wa Kundi C na watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi D.
No comments:
Post a Comment