BUKOBA SPORTS

Wednesday, January 28, 2015

KADI NYEKUNDU YA CRISTIANO RONALDO AFUNGIWA MECHI MBILI(2).

Cristiano Ronaldo, amepewa Adhabu ya Kifungo cha Mechi 2 baada ya kupewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Teke Edimar wa Cordoba wakati wa Mechi ya La Liga ambayo Real walishinda 2-1 Jumamosi iliyopita.
Kifungo hicho kitamfanya Ronaldo, mwenye Miaka 29, kuzikosa Mechi za Real Madrid za La Liga dhidi ya Real Sociedad, inayyongozwa na Meneja wa zamani wa Man United David Moyes, na ile na Sevilla lakini atarudi dimbani kwenye Dabi ya Jiji la Madrid dhidi ya Mahasimu wao Atletico Madrid hapo Februari 7.
Mara baada ya Mechi na Cordoba, Ronaldo, akitumia Mitandao ya Kijamii aliomba radhi kwa kutolewa nje huku Mpinzani wake, Edimar, aliemchezea Rafu akimsamehe Ronaldo na kulitaka LFP, Shirikisho la Soka la Spain, kutompa Adhabu kali Ronaldo.
Hiyo ilikuwa ni Kadi Nyekundu ya 4 kwa Ronaldo kwenye La Liga tangu ahamie Real Mwaka 2009 akitokea Manchester United.

No comments:

Post a Comment