BUKOBA SPORTS

Wednesday, January 28, 2015

FA WAMSHITAKI DIEGO COSTA KWA KUCHEZA RAFU UWANJANI.

Diego Costa amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa Kosa la Mchezo wa Vurugu kufuatia vitendo vyake kwenye Mechi ya Marudiano ya Nusu Fainali ya Capital One Cup na Liverpool Uwanjani Stamford Bridge Jumanne Usiku.
Kwenye Mechi hiyo ambayo Chelsea waliifunga Liverpool 1-0 na kutinga Fainali, Costa ameshitakiwa kwa kumtimba kwa makusudi Beki wa Liverpool Emre Can katika Dakika ya 12 ya Mechi hiyo.

Ikiwa atakiri Kosa lake, Costa atafungiwa Mechi 3 kuanzia ya Jumamosi dhidi ya Mabingwa wa England, Manchester City, Uwanjani Stamford Bridge.
Costa amepewa hadi Alhamisi Januari 29, Saa 3 Usiku kukana au kukiri Kosa.

No comments:

Post a Comment