Kwenye Mechi hiyo, Van Gaal alianza na Mfumo wa 3-5-2, ambao hutumia Masentahafu Watatu, na ngoma ilipokuwa Sare 0-0 hadi Mapumziko Mashabiki walisikika wakiimba kutaka 4-4-2.
Kipindi cha Pili Van Gaal alimtoa Beki Jonny Evans na kumwingiza Straika Chipukizi James Wilson na Mfumo kurudi 4-4-2 na Dakika Moja baadae Marouane Fellaini, aliengizwa pia Kipindi cha Pili, akaipa Man United Bao la Kwanza.
Bao la Pili lilifungwa mwishoni na James Wilson.
Van Gaal ameeleza: “Inabidi niwaangalie Wachezaji na kuzungumza nao na kuwapima. Siwezi kuwaangalia Mashabiki kwani Manchester United ina Mashabiki wangapi? Dunia nzima tuna Mashabiki 600 Milioni. Huwezi kuchukua maoni ya Watu 600 Milioni. Kuwaangalia Wachezaji, kuongea nao, kuchambua na kadhalika, hiyo ndio kazi yangu kama Meneja.”
Aliendelea: “Kabla ya Mechi nakuwa tayari nimeshaamua Mfumo upi tutatumia. Nawaangalia Wachezaji Mazoezini na napima Plani yangu ya Mechi kisha naamua na hilo hutokana na nini kimejiri Mazoezini.”
No comments:
Post a Comment