BUKOBA SPORTS

Tuesday, January 20, 2015

EVERTON 0 vs 0 WEST BROMWICH ALBION, MIRALLAS AIKOSESHA EVERTON POINTI TATU KWA KUKOSA PENATI USIKU HUU!! NGOMA YAMALIZIKA KWA SARE YA 0-0.


Gareth Barry wa Everton akichuana vikali na mchezaji wa West Brom James Morrison

Wakicheza kwao Uwanja wa Goodison Park, Everton, katika Dakika ya 44, walikosa kufunga Penati iliyopigwa na Kevin Mirallas na kugonga Posti na kutoka.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Joleon Lescott, Mchezaji wa zamani wa Everton, kuunawa Mpira lakini cha kushangaza ni kwa nini Mirallas alipiga Penati hiyo wakati mpigaji wao wa kawaida, Leighton Baines, alikuwemo Uwanjani.
Wakati huo, Mirallas, Mchezaji wa Kimataifa wa Belgium, alilazimisha kupiga Penati hiyo licha ya wenzake, Romelu Lukaku na Steven Naismith, kumsihi ampe tena Mpira Leighton Baines apige Penati hiyo.
Baines ndie Mpigaji Penati na Frikki maalum wa Everton na amefunga Penati 15 kati ya 16 alizopiga kwenye Mechi za Ligi Kuu England.
Wachambuzi huko England wamemchanachana Mirallas na Gary Neville wa Sky Spotrs TV alieleza kitendo hicho ni skandali.
Neville ameeleza: “Ikiwa ameenda kinyume na matakwa ya Timu au amri ya Meneja hicho ni kitendo kibovu mno. Unaweza kumpiga Mtu ngumi au kumvunja Mtu Mguu, kitu ambacho si lazima, lakini kukiuka amri ya Timu ni kitu kibaya zaidi!”
Nae Mchambuzi mwenzake Neville wa Sky Sports, Jamie Carragher, amedai Mirallas inabidi atafute Klabu nyingine.
Hata hivyo, Meneja wa Everton, Roberto Martínez, amepooza skandali hilo ingawa amekiri Mirallas kukosa Penati hiyo kuliathiri morali ya Timu.
 VIKOSI:
Everton XI:
Joel, Stones, Jagielka, Baines, Coleman, Besic, Barry, Barkley, Naismith, Mirallas, Lukaku
Everton Akiba: Griffiths, Hibbert, Oviedo, Kone, Garbutt, Alcaraz, McAleny
West Brom XI: Foster, Wisdom, McAuley, Lescott, Baird, Gardner, Brunt, Yacob, Morrison, Anichebe, Berahino
WBA Akiba: Myhill, Pocognoli, Dawson, Dorrans, Sessegnon, Samaras, Ideye


No comments:

Post a Comment