HABARI kutoka Nigeria zimesema mwigizaji maarufu wa kiume wa sinema nchini humo, Muna Obiekwe, amefariki jana katika hospitali ya Festac, jijini Lagos, baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa figo. Mojawapo ya filamu aliyocheza Muna. Vyanzo vilivyokuwa karibu na mwigizaji huyo, vinasema Muna alikuwa akipambana na matatizo ya figo ambayo alikuwa ameyafanya siri kwa muda mrefu kabla ya kumwambia rais wa chama cha waigizaji cha Nigeria (AGN), Ibinabo Fiberesima, ambaye aliendelea kuwa karibu naye.
No comments:
Post a Comment