
Kwa City hili ni pigo kubwa hasa baada ya kuwa na wimbi la Mechi 12 bila kufungwa na hasa ukizingatia Mechi yao inayofuata ya Ligi ni ya Ugenini hapo Januari 31 huko Stamford Bridge dhidi ya Chelsea.
Ushindi huu wa Arsenal ulianza kwa Penati laini aliyotoa Refa Mike Dean baada ya kuamua Vincent Kompany amemchezea Faulo Nacho Monreal na Santi Cazorla kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 24.
Arsenal walifunga Bao lao la Pili Dakika ya 66 baada ya Frikiki ya Cazorla kuunganishwa kwa Kichwa na Olivier Giroud.

2-0
Olivier Giroud anaipatia bao la pili Arsenal na kufanya 2-0 dhidi ya man City kwenye Uwanja wa Etihad na analiona lango hilo kwa bao la kichwa baada ya kupata mpira kutoka kwa Santiago Cazorla
Kipigo hiki cha City kimewabakisha walipokuwa kwenye nafasi ya pili huku Arsenal wakipanda hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 39 nyuma ya pointi 1 juu ya Man United wenye pointi 40. Mtanange unaofuata kwa Man City ni Vinara Chelsea wiki ijayo.
1-0 Arsenal wanaongoza kipindi cha kwanza
Santi Cazorla aliipatia bao la kuongoza Arsenal kwa mkwaju wa penati katika dakkika ya 24 kipindi cha kwanza. Kompany ndie aliyeleta shida kwa kumwangusha mchezaji wa Arsenal Nacho Monreal katika eneo hatari.

Wachezaji wa City wakipasha. Kompany kuanza mtanange huu dhihi ya Arsenal

Mashabiki wakiingia uwanjani Etihad tayari kwa mtanange wa kukata na shoka kati ya Wenyeji Man City na Arsenal. Macho ya wengi yanaangalia mastraika Serguo Aguero wa City na Alexis Sanchez wa Gunners.

No comments:
Post a Comment