BUKOBA SPORTS

Thursday, February 5, 2015

AFCON 2015: CONGO DR 1 vs 3 IVORY COAST, YAYA TOURE, GERVINHO NA KANON WAIPELEKA TIMU YAO FAINALI.

Ivory Coast imekuwa ya kwanza kutinga Fainali ya Mashindano YA Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, baada ya Jana Usiku huko Estadio de Bata, Mjini Bata, Nchini Equatorial Guinea, kuichapa Congo DR Bao 3-1.
Ivory Coast walitangulia kufunga Dakika ya 21 kwa Bao la Yaya Touré ambae aliwasha Shuti la Mita 20 na kumwacha Kipa machachari Kidiaba akitapatapa.
Congo DR walisawazisha kwa Penati ya Dakika ya 24 iliyotolewa baada ya Bailly kuunawa Mpira na Mbokani kufunga.
Lakini Ivory Coast walienda mbele 2-1 katika Dakika ya 41 kwa Bao la Gervinho aliepokea pasi ya Bony.
Hadi Mapumziko Ivory Coast 2 Congo DR 1.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 68, Wilifried Kanon aliipa Ivory Coast Bao la 3 na kutinga Fainali kwa Bao 3-1.
Alhamisi ni Nusu Fainali nyingine kati ya Wenyeji Equatorial Guinea na Ghana.
Kocha wa Ivory Coast Herve Renard

No comments:

Post a Comment