BUKOBA SPORTS

Thursday, February 5, 2015

VAN GAAL ABANWA NA FA, MATAMSHI YAKE KUYATOLEA UFAFANUZI LEO"

MENEJA Manchester United Louis van Gaal amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa matamshi yake aliyoyatoa walipotoka Sare 0-0 na Cambridge United huko Abbey Stadium kwenye Mechi ya Raundi ya 4 ya FA CUP Mwezi uliopita. 
Baada ya Mechi hiyo, Van Gaal aliongea: “Najua kwenye Mechi kama hizi kila kitu kinakupinga. Washabiki, Kiwanja na Difensi yao. Hata Refa, mlimwona. Kila kitu unachoweza kufikiria kinakupinga. Cambridge ni Timu dhaifu, kila Mtu anajua hilo, na lazima ujue namna ya kuwafunga. Lakini mara nyingi unashindwa. Kwa bahati bado tupo FA CUP. Tunacheza Nyumbani na lazima tuwafunge!”

Leo FA imetoa Taarifa kuwa kauli ya Van Gaal kuhusu Refa Chris Foy ni kinyume na Kanuni kwani inamaanisha Refa huyo alipendelea.
Van Gaal amepewa hadi Saa 3 Usiku Jumatatu Februari 9 kujibu Mashitaka yake.
kwenye Marudiano, Man United iliitandika Cambridge United Bao 3-0 na kutinga Raundi ya 5 ya FA CUP na itacheza Ugenini na Preston North End hapo Februari 16.

No comments:

Post a Comment