BUKOBA SPORTS

Sunday, March 29, 2015

JUMANNE TENA ENGLAND UWANJANI KUWAKABA KOO ITALY, WALCOTT, RAHEEM STERLIN NA JAMES MILNER KUIKOSA MECHI HIYO HUKO TURIN!

Kocha wa England Roy Hodgson amesema Wachezaji Wanne wataikosa tripu yao kwenda huko Turin kucheza na Wenyeji wao Italy kwenye Mechi ya Kirafiki hapo Jumanne Usiku.

Wachezaji hao ni pamoja na Straika wa Arsenal Danny Welbeck alieumia Goti Ijumaa wakati England inaichapa Lithuania 4-0 na kuzidi kupaa kileleni mwa Kundi E la EURO 2016.
Kocha wa England Roy Hodgson amesema Wachezaji Wanne wataikosa tripu yao kwenda huko Turin kucheza na Wenyeji wao Italy kwenye Mechi ya Kirafiki hapo Jumanne Usiku. Wengine ambao hawatasafiri ni pamoja na Raheem Sterling wa Liverpool mwenye tatizo la Kidole cha Mguu na James Milner wa Man City mwenye maumivu ya Goti.
Pia Fulbeki wa Everton, Leighton Baines, ameruhusiwa kuondoka kwenye Timu na badala yake kuitwa Fulbeki wa Southampton Ryan Bertrand.
England v Italy ni Mechi ya Kirafiki lakini hii Leo Italy wanacheza Mechi yao ya Kundi H la EURO 2016 dhidi ya Bulgaria. 

No comments:

Post a Comment