BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 8, 2015

AFCON 2017: MWENYEJI GABON, TANZANIA YAPANGWA "KUNDI G" KUKUTANA NA WABABE!

www.bukobasports.com
Huko Mjini Cairo, Misri, CAF hii Leo ilifanya Kikao cha kuchagua Mwenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za Mwaka 2017, AFCON 2017, na pia kufanya Droo ya Makundi ya kuchuja ili kupata Nchi 15 ambazo pamojaaaaa na Mwenyeji zitacheza Fainali za AFCON 2017 Januari na Februari 2017.
Gabon, ambayo Mwaka 2012 ilikuwa Mwenyeji mwenza na Equatorial Guinea wa Fainali za AFCON 2012, waliwabwaga Algeria na Ghana na kuchaguliwa kuwa Mwenyeji wa AFCON 2017.
Katika Droo ya Makundi, Tanzania imetupwa Kundi G ambalo ni gumu mno kwani pia zipo Egypt, Nigeria na Chad.
Mechi za Makundi zitaanza Juni Mwaka huu na Nchi 52 kati ya 54 ambazo ni Wanachama wa CAF, ukiziondoa Somalia na Eritrea, zitashiriki.

Washindi 13 wa Makundi pamoja na Washindi wa Pili Bora Wawili, ukiondoa KUNDI I ambalo Wenyeji Gabon wameshirikishwa lakini Mechi zao zinachukuliwa kama za Kirafiki, ndio watatinga Fainali za AFCON 2017. 

DROO KAMILI YA MAKUNDI:
KUNDI A: Tunisia, Togo, Liberia, Djibouti

  • KUNDI B: Democratic Republic of Congo, Angola, Central African Republic, Madagascar
KUNDI C: Mali, Equatorial Guinea, Benin, South Sudan
KUNDI D: Burkina Faso, Uganda, Botswana, Comoros
KUNDI E: Zambia, Congo, Kenya, Guinea Bissau
KUNDI F: Cape Verde, Morocco, Libya, Sao Tome
KUNDI G: Nigeria, Egypt, Tanzania, Chad
KUNDI H: Ghana, Mozambique, Rwanda, Mauritius
KUNDI I: Ivory Coast, Sudan, Sierra Leone, Gabon

No comments:

Post a Comment