BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 8, 2015

YANGA INATISHA!! YAWABUGIZA BAO 8-0 COASTAL UNION YA TANGA LEO, TAMBWE APIGA 'HAT TRICK'. AZAM FC 1-1 NA MBEYA CITY

VINARA wa Ligi Kuu Vodacom Yanga Leo hii wameitekeza Coastal Union Bao 8-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kupaa kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya Mabingwa Watetezi Azam FC ambao nao Leo wamekwaa mkenge wa Mbeya City baada kutoka nao Sare ya Bao 1-1.
Huko Uwanja wa Taifa ilikuwa burudani tupu kwa Washabiki wa Yanga ambao Wikiendi iliyopita walisheherekea Timu yao kutinga Raundi ya Pili ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho baada ya kuibwaga FC Platinum kwa Jumla ya Mabao 5-2 katika Mechi mbili.

Leo Shujaa mkubwa wa Yanga alikuwa Mchezaji wa Burundi Amisi Tambwe aliepachika Bao 4 huku Simon Msuva akipiga Bao 2 na nyingine kufungwa na Mchezaji wa Liberia, Kpah Sean Sherman, likiwa Bao lake la kwanza kwenye Ligi, na jingine na Salum Telela.

Nao Azam FC, wakiwa kwao Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, walipiga mkenge baada ya kutoka Sare ya Bao 1-1 na Mbeya City inayopigana kujinusuru kutokumbwa na balaa la kushuka Daraja.

Azam FC walitangulia kufunga kwa Bao la Kipre Balou Dakika ya 61 lakini Dakika 4 baadae Mbeya City walisawazisha kwa Penati ya Raphael Alpha.

Matokeo ya Leo yamewafanya Yanga wawe juu zaidi kileleni wakiwa na Pointi 43 kwa Mechi 20 na Azam FC wakibaki Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 37 kwa Mechi 19.

Kiungo wa Yanga, Salum Telela, akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda 8-0. (Picha na Francis Dande).

Simon Msuva akishangilia bao aliloifungia timu yake.

Wachezaji wa Yanga wakishangilia.

Haruna Niyonzima akiruka kihunzi cha, Hamoud Abdulhalim.

Amis Tambwe akiwatoka wachezaji wa Coastal Union.

Mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Coastal Union ya Tanga, Simon Mbelwa, akimpa ‘tano’ mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, baada ya kuifungia timu yake ‘hat trick’ na kukabidhiwa mpira katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Amis Tambwe akipongezwa na kocha wake.

Amis Tambwe akipongezwa na mashabiki wa Yanga.

Amis Tambwe akichuana na mchezaji wa Coastal Union, Mohamed Ally.
Mashabiki wa Yanga wakishagilia timu yao baada ya kuifunga Coastal Union 8-0.

No comments:

Post a Comment