BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 8, 2015

LA LIGA: BARCELONA 4 vs 0 ALMERIA, LIONEL MESSI, SUAREZ NA MARC BARTRA WAISONGESHA ZAIDI KILELENI BARCA!

BAO za Barcelona zilifungwa na Lionel Messi dakika ya 33 kipindi cha kwanza na Bao la pili lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 55 na Luis Suárez na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya Almeria.Tunateleza tuu kileleni!
Marc Bartra dakika ya 75 aliwaongezea bao Barca na kufanya 3-0 na kwenye dakika za majeruhi dakika ya 90 Luis Suarez aliifungia bao la nne na kufanya 4-0 dhidi ya Almeria na mtanange kumalizika.

Messi akishangilia bao lake wakati wa mtanange wao walipoibwagiza bao 4-0 dhidi ya Almeria usiku huu

Suarez nae katupia bao 2-0 katika Ushindi wa leo dhidi ya Almeria

Marc Bartra nae leo kauona mwezi dakika ya 75 kafunga bao
Mpaka ndani ya Nyavu

Dani Alvesakimpongeza Lionel  Messi alipoifungia Barca bao la kwanza

Messi ametimiza bao 32 kwa msimu huu.

Mchezaji wa Zamani wa Ufaransa na Timu ya Barcelona Eric Abidal (katikati) alishuhudia live mtanange huo kwenye Uwanja wa Nyumbani wa Barca Nou Camp.

No comments:

Post a Comment