BUKOBA SPORTS

Saturday, April 11, 2015

ANDY MURRAY AND KIM SEARS WEDDING

Andy Murray na Kim Sears
Mwishoni mwa wiki hii, kulikuwa na shamra shamra kwa mcheza tenis maarufu ulimwenguni Andy kupata kujiko,wakati huo huo Bibi na Babu wa mcheza tennis huyo raia wa Uingereza Andy Murray, wamesema kuwa harusi ya mjukuu wao ilikuwa ya kukata na shoka na kufana mno. Bibi Shirley Erskine na mumewe Roy Erskine walikuwa ndio watu wa kwanza kucheza dance la wawili wawili katika harusi hiyo iliyofanyika April 11, ambapo Murry aliuaga ukapera kwa kumuoa Kim Sears.

Mcheza tennis Andy anayeshika nafasi ya tatu duniani kwa ubora katika mchezo huo, alishindwa kujizuia na kujikuta akiangusha chozi la huba wakati akiingia katika lango kuu la kanisa kuu la Dunblane,kwenda kula kiapo na mpenzi wake wa siku nyingi Kim.
Andy Murray

Ross Hutchins

Judy Murry arrives for the Wedding of her son

No comments:

Post a Comment