BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 15, 2015

AZAM FC WABANWA MBAVU TENA LEO, WATOKA 0-0 NA MGAMBO JKT, MTIBWA 1 vs 0 TANZANIA PRISONS

Mabingwa Watetezi Azam FC Leo tena wameendelea polepole kuuacha Ubingwa wao ukielekea Jangwani kwa Yanga baada ya kutoka Sare 0-0 na Mgambo JKT hukoo Mkwakwani, Tanga.
Hii ni Sare ya 3 mfululizo kwa Azam FC baada ya kutoka Droo 1-1 na Mbeya City na Mtibwa Sugar.
Huko Manungu, Morogoro, Wenyeji Mtibwa Sugar waliichapa Tanzania Prisons Bao 1-0 na kujikwamua kutoka Timu za mwishoni mwa Ligi.
Bao la ushindi la Mtibwa lilifungwa na Kepteni wao Shaban Nditi kwa Penati iliyotolewa baada ya Straika wao Mussa Mgosi kuchezewa Faulo.

No comments:

Post a Comment