BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 21, 2015

CARLO ANCELOTTI: TUTAPAMBANA KUFA NA KUPONA DHIDI YA ATLETICO MADRID LICHA YA KUANDAMWA NA MAJERUHI!!

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti ana uhakika kikosi kiko imara kukabiliana na mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kesho. Kikosi cha Madrid kinakabiliwa na nyota kadhaa majeruhi akiwemo Luka Modric, Gareth Bale na Karim Benzema.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana. Akihojiwa Ancelotti amesema hana shaka sana kuelekea katika mchezo huo utakaofanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu pamoja na majeruhi alionao. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anadhani Isco ataweza kuiziba nafasi ya Modric katika nafasi ya kiungo huku Jese na Chicharito wakitarajiwa kuziba nafasi za Benzema na Bale.

No comments:

Post a Comment