BUKOBA SPORTS

Friday, April 17, 2015

DAKTARI BAYERN MUNICH AJIUZULU BAADA KICHAPO CHA 3-1 KUTOKA KWA FC PORTO!

Daktari wa Bayern Munich Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt amejiuzulu wadhifa wake wa Miaka 38 baada ya Idara yake ya Tiba kulaumiwa kwa Timu hiyo kuchapwa 3-1 huko Ureno na FC Porto hivi Juzi katika Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Kwenye Mechi hiyo, Bayern iliwakosa Nyota wake kadhaa ambao walikuwa Majeruhi.
Dakta Muller-Wohlfahrt, mwenye Miaka 72, amesema: "Kwa sababu zisizoelezwa, Idara ya Tiba ndio imelaumiwa sana na kufungwa. Uhusiano wa kuaminiana sasa umeharibiwa moja kwa moja!"
Kwenye Mechi hiyo, Bayern iliwakosa Mawinga wao Franck Ribery na Arjen Robben, Kiungo Bastian Schweinsteiger na Beki David Alaba.
Kocha wa Bayern, Pep Guardiola, alisikika akihoji iweje Mchezaji wa Kimataifa wa France, Ribery, awe nje toka Machi 11 akiuguza Enka wakati waliambiwa atakuwa nje kwa Siku chache tu.Dakta Muller-Wohlfahrt, ambae ameshawahi pia kuwa Daktari wa Timu ya Taifa ya Germany, anasifika kwa kuganga Wanamichezo maarufu Duniani akiwemo Bingwa wa Dunia na Olimpiki, Mkimbiaji Usain Bolt.
Bingwa wa Dunia na Olimpiki, Mkimbiaji Usain Bolt
Bayern ndio Mabingwa wa Germany na wanaongoza Ligi ya Bundesliga wakiwa Pointi 10 mbele na pia wapo Nusu Fainali ya Kombe la Germany, DFB-POKAL, ambalo walitetea na watacheza na Borussia Dortmund.
Bayerb watarudiana na FC Porto Wiki ijayo huko Allianz Arena Jijini Munich.


Pep Guardiola amedai kuwa yeye ataendelea kuiongoza Bayern msimu ujao licha ya Dokta kuachia kibarua chake.

No comments:

Post a Comment