BUKOBA SPORTS

Saturday, April 18, 2015

JULIO AWAAMBIA WACHEZAJI WAKE, HAKUNA KUBWETEKA!! LEO NI USHINDI TUU!

Wachezaji wa Coastal Union wakipata darasa kutoka kwa Kiongozi (Meneja) wa Klabu hiyo ya Tanga Jamhuri Kihwelo wakati wa Mazoezi yao.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ amewaambia wachezaji wake wanatakiwa kufanya kila linaliwezekana kuhakikishaw anashinda mechi yao inayofuata.
Coastal Union itakipiga dhidi ya Polisi Moro ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Julio amewaambia wachezaji wake mara tu baada ya kumaliza mazoezi kwamba ni lazima washinde na hawatakuwa na sababu ya kujitetea.
“Hatuna cha kusema kama sababu ya kupoteza, kikosi chetuni imara na ushirikiano tunaopata ni mkubwa. Hivyo tupambane na kuibuka na ushindi. “Ushindi dhidi ya Polisi ndiyo utakuwa dira kuwa mechi zilizobaki tunamaliza kwa staili ipi,” alisema Julio.
Coastal Union ilikuwa inakwenda mwendo wa kusuasua. Lakini imeonekana kuanza kuamka huku baadhi ya wadau akiwemo Nassor Bin Slum wakirejea kuungana na wenzao kuisaidia isiporomoke hadi daraja la kwanza.

No comments:

Post a Comment