BUKOBA SPORTS

Saturday, April 18, 2015

LEO JUMAMOSI HAPATOSHI!! NI YANGA SC vs ETOILE DU SAHEL

Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Jumamosi utakuwa ni dimba la burdani safi ya Mechi kali ya Kimataifa wakati Yanga watakapocheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.
Etoile du Sahel walitua Dar es Salaam Alfajiri ya Ijumaa wakiwa chini ya Kocha wao Faouzi Benzarti na kukataa kuzungumza lolote mbali ya kukiri hawaijui Yanga.
Yanga ndio Klabu pekee ya Tanzania iliyobaki michuano ya Barani Afrika baada ya Azam FC, KMKM na Polisi Zanzibar kutupwa nje mapema.

Na ili kuhamasisha umma wa Tanzania kuishangilia Yanga, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, amekaririwa akisema: "Kama hautaki kuishangilia Yanga au huitakii ushindi Yanga basi tulia Nyumbani!"

Waamuzi wa Mechi hii ni kutoka Msumbiji ambao ni Samwel Chirindza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide na Kamisaa ni kutoka Sudan, Salah Ahmed Mohamed.
Viingilio ni kuanzia Shilingi 5,000 hadi 40,000. 



CAF KOMBE LA SHIRIKSHO
Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya Timu 16

RATIBA
Jumamosi Aprili 18
Young Africans vs E.S. Sahel
Royal Leopards vs AS Vita Club
Warri Wolves vs Etanchéité
Jumapili Aprili 19
CF Mounana vs Orlando Pirates
Al Zamalek vs Fath Union Sport de Rabat
Onze Createurs vs ASEC Mimosas Abidjan 


Marudiano Wikiendi ya Mei 5
Washindi 8 wa Raundi hii watajumuika na Timu 8 zilizobwagwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuwekwa kwenye Droo maalum kupanga Mechi 8 za Mtoano na Washindi wake 8 kutinga hatua ya Makundi ambayo yatakuwa na Makundi mawili ya Timu 4 kila mmoja yatakayocheza Mtindo wa Ligi wa Nyumbani na Ugenini.

No comments:

Post a Comment