
Wachezaji wa Villa wakishangilia Ushindi wao kwenda Fainali Wembley..kukutana uso kwa Uso na Arsenal.
Liverpool wakiongozwa na Nahodha wao Steven Gerrard ambae Leo ni kumbukumbu ya Siku yake ya Kuzaliwa, ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 30 la Philippe Coutinho aliepokea pasi ya Raheem Sterling lakini Dakika 6 baadae Straika wa Aston Villa Christian Benteke alisawazisha Bao hilo baada ya kuikamata pasi safi ya Fabian Delph.
Kipindi cha pili dakika ya 54 Fabian Delph aliwafungia bao la pili Aston Villa na kufanya 2-1.
Coutinho dakika ya 30 anaipachikia bao la kuongoza Liverpool kwa kufanya 1-0 dhidi ya Aston Villa.

Gerrard akipagawa bada ya kipigo hicho.

Steven Gerrard

Ni Homa ya kipigo cha Nusu Fainali Wembley

Christian Benteke aliisawazishia bao Aston Villa kwa kufanya 1-1 katika kipindi hicho cha kwanza dakika ya 36.






Raha ya kupata bao


Hadi Mapumziko Aston Villa 1 Liverpool 1
Kipindi cha Pili, Dakika ya 54, Fabian Delph alianzisha muvu safi na kumpa Benteke aliemsogezea Grealish aliemrudishia Fabian Delph na kupiga Bao la Pili safi na la ushindi.
Fainali ya FA CUP itachezwa Mei 30 Uwanja wa Wembley.












Steven Gerrard ndani
VIKOSI:
Aston Villa: Given, Bacuna, Baker, Vlaar, Richardson, Westwood, Delph, Cleverley, Grealish, N’Zogbia, Benteke
Akiba: Guzan, Okore, Sinclair, Weimann, Cole, Lowton, Gil
Liverpool: Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Moreno, Allen, Henderson, Gerrard, Markovic, Coutinho, Sterling
Akiba: Jones, Johnson, Toure, Lambert, Manquillo, Borini, Balotelli
Mashabiki wa Villa wakiingia Uwanjani Wembley.
No comments:
Post a Comment