Kipindi cha pili dakika ya 45 walifanya mabadili kwa makini kwa
Sammy Ameobi kumbadili Yoan Gouffran na Gabriel Obertan kumbadili Mehdi Abeid na kupata bao dakika ya mapema bao la kusawazisha katika dakika ya 46 kwa kufanya 1-1 bao lililofungwa na Jack Colback.
Dakika ya 53 Spurs walipiga mpira wa adhabu frii kiki na kuzama moja kwa moja ndani ya lango la Newcastle United na kujipatia bao la kuongoza la pili, Frii kiki iliyopigwa na Christian Eriksen na kufanya 2-1.
Bao la mwisho la tatu kwa Spurs lilifungwa na Staa wao wa mabao Harry Kane katika dakika ya majeruhi na mtanange kumalizika kwa 3-1 dhidi ya Newcastle United. Harry Kane akifikisha jumla ya mabao 20 msimu huu.
No comments:
Post a Comment