
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia baada ya kuibuka na pointi 3 muhimu dhidi ya Man United.

Chelsea ikiwa watashinda Mechi zao 2 zinazofuata basi wao ni Mabingwa.

Ubingwa ni wa kwetu!!

Fellaini akifanya yake

Rooney akipata maelezo juu ya rafu kwa Falcao

John Terry akigombea mpira wa kichwa kupitia kona

Kocha Jose Mourinho
Ushindi huu umewapa Chelsea uongozi wa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Arsenal na Man United kubaki Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 11 nyuma.
Chelsea walifunga Bao lao la ushindi Dakika ya 38 kupitia Eden Hazard baada ya pasi nzuri ya kisigino ya Oscar kwenye Mechi ambayo Man United walimiliki Mpira kwa Asilimia 70 dhidi ya 30 ya Chelsea.
Katika Dakika za mwishoni Refa Mike Dean aliinyima Man United Penati baada ya Ander Herrera kuangushwa ndani ya Boksi na badala yake kumpa Kadi ya Njano.
Eden Hazard dakika ya 38 kipindi cha kwanza aliipatia bao la kuongoza kwa kufanya 1-0 dhidi ya Manchester United. Baaada ya kupata pasi safi ya kisigino kutoka Oscar na kumfunga kipa wa Man United De Gea na mechi kwenda mapumziko Chelsea wakiongoza. 
Eden Hazard akipongezwa na Mashabiki kwa kufanya 1-0

Hazard chupuchupu apate bao tena


Ander akimbana Cesc Fabrigas

Mwamuzi akizungukwa na wavchezaji wa Man United juu ya rafu

Fellaini na Zouma

Ander na Cesc

Drogba kwenye patashika

Drogba dhidi ya Ander Herrera

Mashabiki wakiwa tayari kwa mtanange huu wa Chelsea vs Man United
VIKOSI:
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Terry, Cahill, Azpilicueta, Zouma, Matic, Oscar, Fabregas, Hazard, Drogba.
Akiba: Cech, Luis, Ramires, Mikel, Willian, Cuadrado, Solanke.
Man Utd: De Gea, Valencia, Smalling, McNair, Shaw, Rooney, Mata, Ander Herrera, Fellaini, Young, Falcao.
Akiba: Da Silva, Di Maria, Januzaj, Van Persie, Valdes, Blackett, Pereira.
Refa: Mike Dean.
Msimamo ulivyokuwa kabla ya Mtanange huu.
No comments:
Post a Comment