BUKOBA SPORTS

Saturday, June 13, 2015

EURO 2016: BALE AIPA USHINDI WALES DHIDI YA BELGIUM!

Mechi za Makundi ya kufuzu kucheza EURO 2016, Fainali za Mataifa ya Ulaya huko France Mwakani, Jana na Staa wa Real Madrid, Gareth Bale, kuipa ushindi Wales wa 1-0 dhidi ya Timu ya Pili kwa Ubora Duniani, Belgium.
Bao pekee la Mechi hiyo lilifungwa na Bale katika Dakika ya 25 baada ya Kichwa kilichopoteza mwelekeo cha Mchezaji wa Belgium, Radja Nainggolan, kumkuta na kuukwamisha Mpira wavuni.
Ushindi huu umeifanya Wales ipige hatua kubwa ya kufuzu kucheza Fainali za EURO 2016, ikiwa ni mara yao ya kwanza katika Miaka 57 kucheza Fainali za Mashindano makubwa kwani sasa wapo kileleni mwa Kundi B wakiwa Pointi 3 mbele ya Belgium na Pointi 5 nyuma ya Timu ya 3 Israel.
Mechi za Makundi ya EURO 2016 zitaendelea tena Leo na Kesho.

No comments:

Post a Comment