BUKOBA SPORTS

Saturday, June 20, 2015

FULL TIME: TANZANIA 0 vs 3 UGANDA, KIPIGO TENA KWA STARS!!

Taifa Stars imeendelea kupigwa kama tulivyozoea baada ya kufungwa 3-0 na Uganda katika Mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali ya kufuzu kucheza Fainali za CHAN 2016 iliyochezwa Amaan Stadium, Zanzibar Usiku huu.
Hadi Mapumziko, Uganda, chini ya Kocha kutoka Serbia, Milutin ‘Micho’ Sredojevic, walikuwa mbele kwa Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 39 Mfungaji akiwa Erisa Sekisambu.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 65 alikuwa tena Erisa Sekisambu aliewapa Uganda Bao lao la Pili na Bao la 3 kufungwa kwa Penati ya Farouk Miya katika Dakika ya 85.
Timu hizi zitarudiana huko Kampala baada ya Wiki mbili na Mshindi atakutana na Sudan katika Mechi ya Raundi ya Mwisho ya Mtoano na atakaeibuka kidedea ndio atatinga Fainali za CHAN 2016 zitakazochezwa Nchini Rwanda Mwakani.
VIKOSI:
TAIFA STARS:
Deogratias Munishi, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Salum Mbonde, Jonas Mkude, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba, Kelvin Friday, Simon Msuva
Akiba: Mwadini Ali, Hassan Isihaka, Mwinyi Hajji, Said Juma, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa, John Bocco
UGANDA: James Alitho, Dennis Okoth, Brian Ochwo, Hassan Waswa , Shafiq Bakaki, Derick Tekkwo, Muzamil Mutyaba, Erisa Sekisambu , Farouk Miya, John Semazi, Robert Sentongo
Akiba: Brian Bwete, Deus Bukenya, Keziron Kizito, Yasser Mugerwa, Martin Kizza, Frank Kalanda, Fahad Muhammed
REFA: Hudu Munyeme (Rwanda)

No comments:

Post a Comment