BUKOBA SPORTS

Sunday, July 12, 2015

UHAMISHO: GLEN JOHNSON AJIUNGA NA KLABU YA STOKE CITY

Stoke City wamefanikiwa kupata saini ya Mchezaji wa zamani wa Liverpool Glen Johnson.
Beki huyo, mwenye Miaka 30 alietemwa na Liverpool, amejiunga na Stoke City kama Mchezaji Huru na kusaini Mkataba wa Miaka Miwili ambao una Nyongeza ya Mwaka mmoja zaidi.
Akiupokea kwa furaha ujio wa Beki huyo wa Kimataifa wa England, Meneja wa Stoke, Mark Hughes, alisema: "Ni nyongeza nzuri sana kwetu. Ni Beki mwenye kipaji na hufunga pia."

Glen Johnson, ambae ni Fulbeki wa Kulia, alijiunga na Liverpool Mwaka 2009 kutoka Portsmouth kwa Ada ya Pauni Milioni 17.5.
Pia ameichezea England Mechi 54 kati ya 2003 na 2014.
Sasa Johnson atajiunga na wapya wengine wa Stoke City ambao ni Marco van Ginkel, Shay Given, Joselu, Philipp Wollscheid na Jakob Haugaard.
Glen Johnson

No comments:

Post a Comment