UHAMISHO: KLABU YA PSG BADO INASISITIZA INAMHITAJI ANGEL DI MARIA WA MAN UNITED!
Kocha wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc ametoboa kuwa Klabu yao wana nia ya kumchukua Winga wa Argentina anaechezea Manchester United, Angel Di Maria.
Hata hivyo, Kocha huyo, ambae aliwahi kuichezea Man United, amekiri Uhamisho huo utakuwa mgumu kutokana na Dau ambalo litatakiwa kulipwa.
Di Maria, ambae alitua Man United Msimu uliopita kwa Ada kubwa iliyovunja Rekodi huko Uingereza ya Pauni Milioni 59.7, alianza kwa makeke huko Old Trafford lakini baadae akafifia na kushindwa kupata namba katika Kikosi cha Kwanza cha Meneja Louis van Gaal.
Kabla Di Maria kuhamia Man United, PSG pia ilitaka kumnunua lakini walikwama kutokana na kubanwa na Adhabu ya UEFA ya kutonunua Wachezaji baada ya kukiuka Kanuni za FFP [Financial Fair Play] ambazo hutaka Klabu ziwe na Matumizi yanayotokana na Mapato yao wenyewe tu.
No comments:
Post a Comment