BUKOBA SPORTS

Sunday, August 2, 2015

UZINDUZI WA ALBAMU TATU ZA MWAITEGE NI KESHO(LEO) UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE, WAIMBAJI WATAKAO MSINDIKIZA WATAMBULISHWA


Mwimbaji wa nyimbo za injili, Boniface Mwaitege (katikati), akiimbaji sanjari na waimbaji wenzake wakati wakitambulishwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi. Waimbaji hao kesho watatoa burudani wakati wakimsindikiza mwimbaji mwenzao Boniface Mwaitege katika uzinduzi wa albamu zake tatu za Utanitambuaje, Mama ni mama na Tunapendwa na Mungu utakaofanyika kesho ukumbi wa Diamond Jubilee saa nane mchana kesho. Kutoka kulia ni Faustine Mnishi, Upendo Kilahiro, Jesca Magupa (BN) na Atosha Kissava.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya uzinduzi huo.
Msama (katikati), akiwa na waimbaji watakaotoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
MWANAMUZIKI wa Injili, Boniface Mwaitege kesho mchana anatarajiwa kuzindua albamu zake tatu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam leo mchana Mkurugenzi wa Kapuni ya Msama Promotion alisema kuwa maandalizi yote muhimu ya tamasha hilo litakalofanyika kuanzia saa nane mchana yamekamilika, Mwaitege atatambulisha albamu hizo kwa kusindikizwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili.
Alisema mashabiki wa muziki wa Injili watarajie burudani ya nguvu kutokana na maandalizi ya nguvu na ya kipekee aliyofanya mwanamuziki huyo ikiwemo kurekodi albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Nairobi na Kenya.
"Maandalizi yote ya uzinduzi wa albamu za Mwaitege yamekamilika, mashabiki watarajie burudani ya nguvu, pamoja na ujumbe kutoka katika nyimbo hizo pamoja na mwanamuziki wengine watakamsindikiza," alisema Msama.

Alisema sehemu ya mapato katika uzinduzi huo ambao pia utafanyika katika mikoa mingine, itapelekwa kwa kwenye vitu vya watoto yatima.
Msama alizitaja albamu hizo ni pamoja na 'Tunapendwa na Mungu' yenye nyimbo za 'Tukiimba Mungu anashuka', 'Mtoto wa mwenzio ni wako', 'Safari Bado', 'Tumekuja Kukuchukua (Bibi harusi)', 'Tuko Salama', 'Moyo wa Shukrani', 'Hakuna Ridhiki', albamu nyingine ni Utanitambuaje na Mama ni Mama.

Baadhi ya wanamuziki watakaopanda jukwaani kusindikiza uzinduzi wa albamu za Mwaitege waliotambulishwa kwa waandishi wa habari na baadhi ya nyimbo zao zilizotamba katika mabano ni Upendo Kilahiro (Baba Ninakuabudu), Jesca Magupa (Napokea), Mchungaji Faustine Munishi (Malebo) na Atosha Kisava (Umwema).
Akizungumzia utambulisho wa albamu zake tatu, Mwaitege alisema amejiandaa vizuri kwa uzinduzi huo, ambapo mashabiki wataweza kupata burudani nzuri na ujumbe, pia albamu hizo zitakuwepo ukumbini.
Aliwataka mashabiki kufika kwa wingi katika onesho hilo ili kumpa hamasa yeye na waimbaji wengine ambao watamsindikiza.
Awali wasanii wengine waliotajwa kusindikiza uzinduzi huo ni pamoja na John Lisu, Martha Mwaipaja, Faustine Munishi, Upendo Nkone, Christopher Mwahangila, Eiphraim Sekereti, Atosha Kisava, Mess Chengula, Eveline Kabwemela, Ambwene Mwasongwe na Joshua Mlelwa.
Onesho hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini.
Kiingilio katika onesho hilo kitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti maalumu, sh. 5,000 na sh.2,000 kwa watoto.

No comments:

Post a Comment