BUKOBA SPORTS

Sunday, September 27, 2015

UPENDO NKONE KUZINDUA ALBAMU YA TANO LEO!


Uendondo Nkone (katika) akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano na waandashi wa habari kuhusu kuadhimishi miaka 10 tangu aanze huduma ya uimbaji.
NA MWANDISHI WETU
MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za injili nchini Upendo Nkone, kesho anatarajiwa kuadhinisha miaka 10 tangu aanze huduma hiyo ya uimbaji sambamba na uzinduzi wa albamu yake ya tano iitwayo ‘Omba Yesu Anasikia’ yenye jumla ya nyimbo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Nkone alisema mbali ya tukio hilo la kesho kubeba uzinduzi wa albamu mpya na maadhimisho ya miaka yake 10 katika huduma hiyo, pia kwake ni kumshukuru Mungu kujamlia uzima na afaya.
Alisema kudumu kwa miaka yote hiyo katika huduma hiyo yenye vikwazo na hila za kila aina, ni jambo la kumshuruku Mungu ikiwemo kumvusha salama katika matatizo ya kiafya aliyopata mwaka jana hadi kufanyia upasuaji mkubwa.
“Upendo wa Mungu ni mkubwa mno kwangu. Kufanya huduma hii ya uimbaji kwa miaka yote hii 10, sio kitu kidogo. Lakini pia kupitia tukio hili la Jumapili (kesho), nitalitumia kurejesha sifa na utukufu kwa Mungu kunivusha salama katika upasuaji ambao hata madaktari walikiri ulikuwa mgumu,” alisema.
Kuhusu uzinduzi huo utakaofanyika katika ukumbi wa Kanisa la TAG-Upanga lililopo chini ya Askofu Mwasongole, Upendo alisema maandalizi yamekwenda vizuri na atasindikizwa na waimbaji wengi mahiri katika tukio hilo muhimu kwake.

Anawataja baadhi ya waimbaji watakaomshindikiza, ni Bonny Mwaitege, Masanja Mkandamizaji, Messi Chengula, Jesca Boniface Magupa ‘BM’, Bahati Bukuku na wengineo kibao na kutoa wito kwa wapendwa na wapenzi wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi.

Upendo alisema tukio hilo litakaloanza majira ya saa nane mchana, kiingilio cha juu kitakuwa shilingi 5,000 kwa wakubwa na watoto ni shilingi 2000 na kusema kila atakayefika ukumbini, hatajutia muda wake.

Akizungumzia mafanikio ya huduma yake, Upendo amemshukuru Mkurugenzi wa Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama kwa saopoti kwani kupitia matamasha yake ya Pasaka na Krismasi, yamempa nafasi ya kujulikana na kukua zaidi kihuduma.

No comments:

Post a Comment